May 13, 2021 11:53 UTC
  • Wazayuni wakiri kipigo, wameshapata hasara ya dola milioni 160 kwa mashambulio ya muqawama

Chama cha Wazalishaji Bidhaa cha utawala wa Kizayuni kimetangaza kuwa, tangu yalipoanza mashambulizi ya makombora wanamapambano wa Palestina siku chache zilizopita hadi hivi sasa, sekta ya uzalishaji bidhaa ya Israel imeshapata hasara ya dola miliioni 160.

Shirika la habari la FARS limenukuu taarifa ya chama hicho cha wazalishaji bidhaa cha Wazayuni kikiri leo Alkhamisi kuhusu hasara kubwa iliyosababishwa na mashambulio ya makombora ya wanamapambano wa Palesitna na kuongeza kuwa, sekta mbalimbali za uchumi wa Israel zimepata hasara katika mashambulizi ya tangu siku tatu zilizopita ya makombora ya wanamapambano wa Palestina.

Taarifa hiyo imesema pia kuwa, wanamuqawama wa Palestina wameshayapiga kwa makombora 540 maeneo mbalimbali ya kiuchumi ya Israel katika kipindi cha siku tatu zilizopita na kuusababishia utawala huo katili hasara ya dola milioni 160.

Wanajeshi Wazayuni wakiangalia kwa hofu athari za mashambulio ya wanamapambano wa Kisilamu wa Palestina

 

Huku hayo yakiripotiwa, utawala wa Kizayuni umeendeleza jinai zake dhidi ya wananchi wa kawaida wa Palestina na hadi hivi sasa umeshaua makumi ya raia wasio na hatia.

Hadi wakati tunaandaa habari hii, Wizara ya Afya ya Ukanda wa Ghaza ilikuwa imetangaza kuwa, wananchi 72 wa Palestina wameshauawa shahidi kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni. 

Mtandao wa habari wa Shahab News umenukuu taarifa ya wizara hiyo ikisema kuwa, watoto 17 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa shahidi hadi hivi sasa, 388 kati yao wamejeruhiwa, 115 kati ya hao waliojeruhiwa katika mashambulio ya kikatili ya Wazayuni ni watoto wadogo na 50 ni wanawake.

Tags