May 15, 2021 04:29 UTC
  • Netanyahu azishukuru Marekani, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kwa kuunga mkono jinai za Israel

Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amewashukuru na kuwapongeza marais Joe Biden wa Marekani na Emmanuel Macron wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kwa kuunga mkono utawala huo dhalimu katika jinai unazoendelea kufanya dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Netanyahu ametoa shukrani hizo sambamba na kutoa vitisho kwa mara nyingine tena dhidi ya makundi ya muqawama ya Palestina kwa kueleza kwamba, utawala wa Kizayuni utatoa pigo kali kwa makundi hayo.

Waziri Mkuu wa utawala katili wa Israel alitoa kauli hiyo Ijumaa jioni baada ya kikao alichofanya na wakuu wa mashirika ya usalama ya utawala huo wa Kizayuni na kuongeza kwamba jeshi la Kizayuni limezishambulia ngome za chini ya ardhi za makundi ya muqawama ya Palestina na kwamba mashambulio hayo yataendelezwa.

Mashambulio ya kinyama ya Israel Ukanda wa Gaza

Netanyahu ametoa vitisho hivyo katika hali ambayo, Abu Hamza, msemaji wa brigedi za Sarayal-Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amejibu vitisho vya utawala wa Kizayuni vya kuanzisha operesheni ya mashambulio ya nchi kavu dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa kusisitiza kuwa, mapambano ya nchi kavu ni njia ya mkato zaidi kwa muqawama kufikia ushindi na kwamba katika mapigano hayo, hatima ya wanajeshi wa Kizayuni itakuwa ni ima kutekwa au kuuawa.../  

Tags