May 24, 2021 12:49 UTC
  • Hamas yawatahadharisha Wazayuni kuhusu kushambulia tena Quds

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imewatahadharisha Wazayuni maghasibu kuhusu kufanya chokochoko na mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya Quds na Msikiti Mtukufu wa al Aqsa.

Abdul Latif al Futuh, msemaji wa Hamas amesema katika hotuba maalumu kwamba, harakati hiyo iko tayari kukabiliana na njama na mipango yoyote ya adui ya kuwafukuza kwenye nyumba zao wakazi wa kitongioji cha Shekh Jarrah au kuugawa msikiti wa al Aqsa na kubadilisha athari na nembo za Kiislamu. 

Al Futuh ameeleza kuwa, machaguo ya kukabiliana na adui Mzayuni yapo mezani na akasema Hamas inamtahadharisha adui Mzayuni asithutubu kuchukua hatua yoyote itakayoibua upya mapigano na mivutano huko Quds. 

Jana na ikiwa imepita siku mbili tu baada ya kutangazwa usitishaji vita kati ya wanamuqawama na utawala wa Kizayuni, wanajeshi na walowezi wa Kizayuni waliuvamia msikiti wa al Aqsa na kusababisha mapigano makali kati ya raia wa Palestina na wanajeshi wa utawala huo ghasibu. 

Uvamizi wa wanajeshi wa Israel katika msikiti wa al Aqsa  

Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel leo pia wamefanya operesheni kubwa na kuwatia mbaroni Wapalestina 500 ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Kufuatia kitendo hicho, makundi ya muqawama ya Palestina yameionya Israel kwamba muhula wa kusitisha mapigano unakaribia kumalizika na kwamba, mapigano yataanza tena iwapo utawala huo hautawajibika.   

Israel ilianzisha vita dhidi ya raia wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na huko Ghaza tangu tarehe 10 mwezi huu wa Mei; na kumalizika tarehe 21 kufuatia ombi la baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni na upatanishi wa baadhi ya pande ajinabi baada ya kushindwa jeshi la utawala huo kukabiliana na wanamuqawama wa Palestina. 

Tags