Jun 06, 2021 03:12 UTC
  • Raia wa Palestina katika korokoro za Israel
    Raia wa Palestina katika korokoro za Israel

Jumuiya ya Mateka na Wafungwa wa Palestina imetangaza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umewatia nguvuni zaidi ya Wapalestina milioni moja tangu mwaka 1967.

Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Mateka na Wafungwa wa Kipalestina imesema kuwa, elfu 50 kati ya Wapalestina hao waliokamatwa na utawala haramu wa Israel walikuwa watoto, na zaidi na elfu 17 miongoni mwao ni wanawake.

Taarifa hiyo imesema kuwa, Wapalestina waliokamatwa na Israel wanaishi katika mazingira mabaya na magumu sana kwenye jela za utawala huo ghasibu na wanakabiliana na aina mbalimbali za mateso ya kimwili na kiroho. Imesema kuwa katika kipindi hicho mateka 226 wa Kipalestina wameua shahidi katika jela za Israel, 73 miongoni mwao kutokana na mateso na wengine 71 kutokana na kutelekezwa na kunyimwa matibabu. Ripoti hiyo imesema Wapalestina wengine 82 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi moja kwa moja na wanajeshi wa Israel.

Taarifa ya Jumuiya ya Mateka na Wafungwa wa Palestina imesema kuwa mamia ya Wapalestina pia wameaga dunia kipindi kifupi baada ya kuachiliwa huru kutoka kwenye korokoro za Israel kwa kusumbuliwa na athari mbaya za mateso waliyoyapata kwenye jela za utawala huo habithi, na imeitaka jamii ya kimataifa kuvunja kimya chake mbele ya uhalifu na mauaji yanayofanywa na Israel.

Zaidi ya Wapalestina milioni moja walikamatwa na Israel tangu mwaka 1967

Kwa sasa zaidi ya Wapalestina elfu nne na mia nane wanashikiliwa katika jela na korokoro za kutisha za Israel ambako wanakabiliana na sulubu na mateso makubwa. 170 kati ya Wapalestina hao wanaoshikiliwa katika jela za Israel ni watoto wadogo na 39 ni wanawake.    

Tags