Jun 16, 2021 12:23 UTC
  • Uhusiano wa Imarati na Israel wapigwa na dhoruba

Siku chache baada ya kuanza utekelezaji wa makubaliano ya mafuta baina ya Abu Dhabi na Tel Aviv, Waziri wa Mazingira wa utawala haramu wa Israel ametoa mwito wa kufutwa mapatano hayo.

Duru za habari zinaarifu kuwa, Tamar Zandberg, Waziri wa Mazingira wa utawala wa Kizayuni wa Israel ametaka kufutilia mbali makubaliano ya pande mbili ya usafirishaji wa mafuta.

Gazeti la Kizayuni la "Israel Hayom" limeripoti kuwa, hatua ya waziri huyo wa Israel kupinga mapatano hayo siku chache tu baada ya kupasishwa inaashiria kuibuka mgogoro na kuingia doa kwenye uhusiano wa tawala mbili hizo.

Mapatano hayo yameiruhusu UAE isafirishe na kuuza mafuta yake katika soka la kimataifa kupitia ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Mkwaruzano huu umeibuka siku chache baada ya tawala mbili hizo kutangaza kuwa makubaliano hayo yameingia katika hatua ya utekelezaji.

Kuingia ila uhusiano wa Imarati na Israel

Hivi karibuni, Imarati ilifungua rasmi ubalozi wake mjini Tel Aviv, siku chache tu baada ya jinai na mauaji ya kutisha ya zaidi ya Wapalestina 250 wa Ukanda wa Gaza, yaliyofanywa na jeshi katili la Israel. 

Umoja wa Falme za Kiarabu ambayo Septemba mwaka jana ilianzisha uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel ni nchi ya kwanza ya Kiarabu baada ya kipindi cha miaka 26. Baadhi ya tawala za Kiarabu zimefuata mkumbo huo kibubusa.

Tags