Jun 20, 2021 12:25 UTC
  • Wazayuni wakiuhujumu Msikiti wa Al Aqsa
    Wazayuni wakiuhujumu Msikiti wa Al Aqsa

Waloweiz wa Kizayuni wameuhujumu kwa mara nyingine Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huku wakipata himaya ya askari wa utawala haramu wa Israel wakati wakitekeleza jinai hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Felestin al Youm, walowezi wa Kizayuni leo Jumapili waliuvamia Msikiti wa Al Aqsa na kuvunjia heshima eneo hilo takatifu.

Taarifa zinasema Wazayuni hao wenye misimamo mikali waliingia katika maeneo mbali mbali ya wazi katika Msikiti wa Al Aqsa huku wakitoa nara dhidi ya Uislamu. Katika hujuma hiyo Wazayuni walipambana na Wapalestina ambao walikuwa wakiwazuia kutenda vitendo viovu vya kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa.

Utawala pandikizi wa Israel unatekeleza jinai hizo katika hali ambayo, hata makundi ya mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu yameouonya utawala huo kuwa kuendelezwa jinai dhidi ya Quds na wakaazi wake ni jambo ambalo litaibua vita vya kieneo.

Kwa maeneno mengine ni kuwa, jinai za Israel dhidi ya Wapalestina mjini Quds na halikadhalika hujuma dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa hazitaishia tu katika makabiliano ya askari wa Israel na harakati za ukombozi wa Palestina, bali wigo wa mapigano sasa utachukua muelekeo wa kieneo ambapo makundi ya muqawama yatakabiliana ana kwa ana na Israel.

Weledi wa mambo wanaamini kuwa, mapigano ya 'Upanga wa Quds' hivi karibuni katika Ukanda wa Ghaza yameleta mlingano mpya katika eneo hili katika makabiliano na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

 

Tags