Jun 22, 2021 08:17 UTC
  • Muqawama wa Palestina wamtahadharisha tena adui Mzayuni

Brigedi ya Mashahidi wa al Aqsa imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa, muqawama utaanzisha duru mpya ya mapigano na mashambulizi ya roketi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu iwapo utawala huo hautafungua vivuko vya Ukanda wa Ghaza.

Abu Muhammad Msemaji wa Brigedi ya Mashahidi wa al Aqsa amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Israel hauwezi kuendelea kuvifunga vivuko vya Ukanda wa Ghaza na kwamba utagharamika pakubwa kwa hatua yake hiyo. 

Msemaji wa Brigedi ya al Aqsa ametahadharisha kuwa, iwapo utawala wa Kizayuni utaishambulia Ghaza, miji ya kizayuni pia itakabiliwa na mashambulizi ya roketi kutoka kwa wanamapambano wa Brigedi ya al Aqsa na makundi mengine ya muqawama.  

Abu Muhammad ameeleza kuwa, makundi ya muqawama yamemtumia ujumbe adui Mzayuni kupitia kwa wapatanishi na yanasubiri jibu ili kubeba silaha wakati wowote. 

Wanamuqawama wa brigedia za mashahidi wa al Aqsa 

Tor Wennesland Mratibu wa Amani wa Umoja wa Mataifa katika Mashariki ya Kati jana aliwasili Ghaza kwa lengo la kufuatilia baadhi ya mambo na mafaili ya mashambulizi yaliyofanywa na Israel dhidi ya eneo hilo, suala la kufungwa vivuko vya Ghaza na kuimarishwa usitishaji vita kati ya makundi ya muqawama ya Palestina na utawala wa Kizayuni. Akiwa Ghaza, Wennesland  amefanya  mazungumzo na Yahya al Sinwar Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas. 

Tags