Jun 23, 2021 02:27 UTC
  • Yair Lapid
    Yair Lapid

Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel anatazamiwa kufanya safari ya kwanza ya kuutembelea Umoja wa Falme za Kiarabu wiki ijayo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, Yair Lapid anatamiwa kuitembelea UAE Juni 29-30, ambapo ameratibiwa kufungua rasmi ubalozi wa utawala huo wa Kizayuni katika mji mkuu Abu Dhabi, na pia ubalozi mdogo mjini Dubai. 

Hivi karibuni, Imarati ilifungua rasmi ubalozi wake mjini Tel Aviv, siku chache tu baada ya dunia kushuhudia jinai na mauaji ya kutisha ya zaidi ya Wapalestina 250 wa Ukanda wa Gaza, yaliyofanywa na jeshi katili la Israel. 

Umoja wa Falme za Kiarabu ambayo Septemba mwaka jana ilianzisha uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel ni nchi ya kwanza ya Kiarabu baada ya kipindi cha miaka 26. Baadhi ya tawala za Kiarabu kama Sudan, Bahrain na Morocco zimefuata mkumbo huo kibubusa.

Kuimarika uhusiano wa tawala zisizowajali Wapalestina

Katika hatua nyingine, kanali ya televisheni ya Kizayuni ya i24NEWS imesema imekwishapewa leseni na Abu Dhabi  ya kuendesha shughuli zake huko Imarati, na kwamba karibuni hivi itafungua ofisi za shirika hilo mjini Dubai.

Satalaiti ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya Etisalat tayari imeanza kurusha hewani matangazo ya kanali hiyo ya saa 24 ya utawala pandikizi wa Israel unaoua watoto na wanawake wa Kipalestina kila uchao.

Tags