Jul 05, 2021 02:51 UTC
  • Makamanda kadhaa wa al-Qaeda waangamizwa na jeshi la Yemen Bayda

Jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea wananchi limeangamiza wananchama kadhaa wa kundi la al-Qaeda katika Peninsula ya Kiarabu (AQAP), wakiwemo makamanda waandamizi wa genge hilo la kigaidi.

Kwa mujibu wa Press TV, vikosi vya Yemen vimeshambulia ngome na maficho ya magaidi hao katika wilaya ya al-Sawma'ah, mkoani al-Bayda, katikati mwa nchi hiyo ya Kiarabu inayozongwa na vita na mapigano.

Vyanzo vya habari vimeviambia vyombo vya habari vya Yemen kuwa, wanachama wa al-Qaeda pamoja na mamluki kadhaa wa Saudi Arabia wamepata kipigo kikali katika operesheni hiyo ya askari wa Yemen.

Habari zaidi zinasema kuwa, kamanda wa ngazi ya juu wa al-Qaenda aliyejitangaza kuwa Gavana wa Bayda, Abu Dharr al-Tayabi ni miongoni mwa wanachama waandamizi wa kundi la al-Qaeda katika Peninsula ya Kiarabu (AQAP) aliouawa katika operesheni hiyo.

Wapiganaji wa Yemen

Makamanda wengine wa al-Qaeda walioangamizwa katika operesheni hiyo ya Jumamosi ni pamoja na Mohammed Hussein al-Junaidi, kamanda wa genge hilo katika wilaya Mudiyah mkoani Abyan, Tawfiq al-Farawi, Abdul Hakim Mubarak al-Qaisi, na Othman Ahmad Abdullah al-Mushdali.

Haya yamejiri siku moja baada ya Muammar al-Iryani, Waziri wa Habari katika utawala wa rais mtoro wa Yemen, Abd Rabbuh Mansur Hadi, kutangaza kuanza kwa eti operesheni kambambe dhidi ya Jeshi la Yemen pamoja na vikosi vya kujitolea wananchi katika mkoa wa al-Bayda.

Tags