Jul 14, 2021 04:06 UTC
  • Hukumu za kifo nchini Bahrain zaongezeka mara 600 tangu 2011

Utekelezaji wa adhabu ya kifo nchini Bahrain umeongezeka sana katika muongo mmoja uliopita, haswa tangu kulipoanza mwamko wa wananchi katika nchi za Kiarabu mwaka 2011.

Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyochapishwa Jumanne ya jana na jumuiya ya kupambana na adhabu ya kifo na kutetea haki za binadamu ya Reprieve na Taasisi ya Haki na Demokrasia ya Bahrain (BIRD), hukumu za kifo katika kisiwa hicho kidogo cha Ghuba ya Uajemi zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 600, na watu wasiopungua 51 wamenyongwa tangu maandamano dhidi ya serikali yalipoibuka mnamo 2011.

Ripoti hiyo imesema kuwa, watu saba tu walihukumiwa adhabu ya kifo katika muongo mmoja wa kabla yake.

Ripoti hiyo ya pamoja imeashiria kukithiri kwa utumiaji wa mateso, haswa katika kesi za adhabu ya kifo zinazohusiana na "ugaidi" licha ya ahadi zilizotolewa na serikali ya Manama za kurekebisho ya rekodi ya hali ya haki za binadamu nchini Bahrain.

Ripoti hiyo imesema kuwa, asilimia 88 ya wanaume waliouawa nchini Bahrain tangu mwaka 2011 walitiwa hatiani kwa mashtaka ya "ugaidi", na asilimia 100 ya miongoni mwao walisema kuwa waliteswa na kunyanyaswa.

Kwa sasa, wanaume wengine 26 wanakabiliwa na hukumu ya kunyongwa, huku 11 kati yao wakisema waliteswa na mamlaka ya Bahrain. 

Mtawala wa Bahrain akiwa pamoja na rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush

Ripoti hiyo imeibaini kuwa Kamati ya Umoja wa Mataifa Dhidi ya Mateso imeeleza wasiwasi wake juu ya tabia ya "majaji wa Bahrain kukubali ushahidi uliopatikana kwa kukiri watuhumiwa baada ya kulazimishwa" na ilipendekeza kwamba majaji "wanapaswa kushughulikia kesi kwa msingi wa ushhidi uliopatikana baada ya watuhumiwa mbele ya mahakama, kwani ushahidi mwingi unapatikana kupitia njia ya kuwatesa watuhumiwa.

Tangu Februari mwaka 2011, wakati ulipoanza mwamko wa Kiislamu Asia Magharibi, Bahrain imekuwa uwanja wa maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga utawala wa kifalme wa ukoo wa Aal Khalifa.

Wabahraini wanataka kuwepo uhuru, uadilifu, kukomeshwa ubaguzi na kuundwa serikali itakayochaguliwa na wananchi wenyewe.

Tags