Jul 17, 2021 08:13 UTC
  • Jihadul-Islami: Walowezi wa Kizayuni ni walengwa halali wa mashambulio ya wanamuqawama

Msemaji wa harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesisitiza kuhusu haki halali na ya kisheria ya kujihami waliyonayo Wapalestina na akabainisha kwamba, walowezi wa Kizayuni ni walengwa halali kisheria wa muqawama.

T’ariq Silmi amesema, taarifa za vyombo vya habari vya Kiebrania viliyofichua kuwa askari wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni walishirikiana pamoja katika mauaji ya Wapalestina 11 yaliyofanywa mwezi Mei katika eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan ni nyaraka na ushahidi wa wazi wa kuthibitisha hatua na vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi wa Palestina.

Walowezi wa Kizayuni

 

Silmi ameeleza kuwa, jeshi la utawala ghasibu linawasaidia na kuwaunga mkono walowezi wa Kizayuni katika vitendo vya kigaidi wanavyofanya dhidi ya wananchi wa Palestina na akaongeza kwamba, kukiri huko kwa vyombo vya habari vya Israel kunaonyesha kuwa, Wapalestina wanaandamwa na kila aina ya njama za Kizayuni kuanzia mauaji, kuporwa ardhi zao, kuchomwa moto mazao yao ya kilimo, kuvamiwa na kubomolewa nyumba zao pamoja na kunyang’anywa mali zao kwa lengo la kuwahamisha katika ardhi yao…/

 

Tags