Jul 18, 2021 11:24 UTC
  • Mataifa ya Kiarabu yakosolewa kwa kunyamazia kimya matukio ya kuhujumiwa msikiti wa al-Aqswa

Sheikh Ikrima Sabri, Khatibu wa Masjidul-Aqswa amekosoa vikali kimya cha mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuhusiana na matukio ya hujuma na uvamizi dhidi ya msikiti wa al-Aqswa.

Sheikh Sabri amesema kuwa, kile kinachojiri katika msikiti wa al-Aqswa, kuanzia hujuma, uvamizi na kuuvunjia heshima msikiti huo ni jinai kubwa.

Aidha amesema, kuanzia jana Jumamosi wanajeshi wa utawala haramu waa Israel wameshadidisha hatua zao za kuwazuia Wapalestina kuingia katikka msikiti huo kwa ajili ya kutekeleza.

Kadhalika Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa amesema kuwa, inakitisha kuona kuwa, licha ya hujuma na uvamizi huo wa Wazayuni, lakini mataifa ya Kiarabu na Kiislamu yamenyamaza kimya na kutochukua hatua yoyote ya kuutetea na kuunusuru msikiti huo.

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wakivamia msikiti wa al-Aqswa

 

Sheikh Ikrima Sabri amebainisha kwamba, Mwenyezi Mungu anashuhudia na atawahesabia wale wote wanaozembea katika kuutetea na kuunusuru msikiti huu ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu. 

Sheikh Ikrima Sabri ameyataka mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuamka na kuchukua hatua za maana zitakazokomesha hujuma na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msikiti mtakatifu wa al-Aqswa.

Katika upande mwingine, Sheikh Sabri amekosoa vikali ushirikiano wa kiusalama wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala ghasibu waa Israel na kubainisha kwamba, hatua hiyo haikubaliki hata kidogo. Amesema, kuna haja ya kujitenga mbali kabisa na hadaa za kisiasa katika jamii.

Tags