Jul 19, 2021 11:31 UTC
  • Ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni zimeonekana katika anga ya msikiti wa al Aqsa

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, ndege zisizo na rubani za Israel zimeonekana katika anga ya msikiti mtakatifu wa al Aqsa.

Droni hizo za utawala haramu wa Kizayuni leo ziliruka katika anga ya msikiti wa al Aqsa kwa lengo la kuwadhaminia usalama  walowezi wa Kiyahudi ili kuushambulia msikiti huo. Wazayuni wamefanya hivyo katika hali ambayo siku kadhaa zilizopita walowezi wa Kizayuni wameshadidisha mashambulizi dhidi ya msikiti wa al Aqsa kufuatia ombi la makundi yenye kufurutu ada ya Waisraili. Naftali Beneti Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni pia amewaagiza Wazayuni waendelee kuushambulia msikiti wa al Aqsa baada ya kufanya kikao huko Quds na Benny Gantz Waziri wa Vita wa utawala huo ghasibu. 

Idara ya Wakfu wa Kiislamu ya Palestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu imesema kuwa jana Jumapili Wazayuni zaidi ya elfu moja waliushambulia mskititi huo mtakatifu. Wakati huo huo, makundi ya muqawama ya Palestina yameutahadharisha utawala wa Kizayuni kuhusu kushadidisha mashambulizi huko Quds inayokaliwa kwa mabavu dhidi ya msikiti wa al Aqsa na kuwatolea wito Wapalestina kufika kwa wingi na kufanya itikafu msikitini hapo ili kulipigania eneo hilo tukufu mkabala na uvamizi wa walowezi Maghasibu wa Israel.

Uvamizi wa mara kwa mara wa Wazayuni katika msikiti wa al Aqsa  

 

Tags