Jul 21, 2021 02:29 UTC
  • Onyo la mwisho la muqawama wa Palestina dhidi ya Israe: Msivuke mistari yetu myekundu

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusiana na hujuma na uvamizi wake dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa na Baitul-Muqaddas.

Onyo hilo limo katika taarifa iliyotolewa na Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiisloamu ya Palestina HAMAS ambaye amewaonya Wazayuni na kuwataka wasivuke mistari myekundu ya muqawama na Wapalestina.

Ismail Hania sambamba na kutoa mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa kuadhimisha Sikukuu ya Eidul-Adh'ha amesisitiza kuwa, harakati ya muqawama imesimama kidete kutetea haki za taifa la Palestina na kwamba, katika vita vilivyopita vya Seif al-Quds muqawama ulimthibitishia adui nguvu ulionayo.

hania

Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

 

Aidha mkuu huuyo wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameeleza kuwa, njama na uvamizi wa hivi sasa wa Wazayuni ni kujitutumua na kutaka kufunika pigo walilopata na hivyo kufifiza ushindi mkubwa wa Wapalestina.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Tags