Jul 24, 2021 08:07 UTC
  • Muqawama wa Iraq waonya kuweko matokeo mabaya ya kushirikiana kiusalama na Marekani

Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Muqawama ya Iraq imesisitiza juu ya kutoruhusiwa uwepo wa aina yoyote ile wa majeshi ya kigeni katika ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Taarifa ya Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Muqawama ya Iraq imetolewa sambamba na kukaribia kufanyika mazungumzo ya Washington-Baghdad na kusisitiza kwamba, mwanajeshi yoyote yule wa kigeni hapasi kuweko katika ardhi ya Iraq.

Taarifa hiyo imebainisha kwamba, jukumu la kikosi cha anga cha Marekani nchini Iraq si jingine bali ni kulinda na kutetea usalama wa utawala wa Kizayuni wa Israel na wakati huo huo kuyafanyia ujasusi makundi ya muqawama.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Muqawama ya Iraq imesisitiza kuwa, askari wote vamizi katika ardhi yote ya Iraq wanapaswa kuondoka kikamilifu.

Wanajeshi wa Marekani nchini Iraq

 

Kwa upande wake Sayyid Ammar Hakim, Kiongozi wa Mrengo wa Kitaifa wa al-Hikma wa Iraq ameashiria mazungumzo ya kistratejia baina ya Washington na Baghdad na kubainisha kwamba, mazungumzo hayo yanapaswa kupelekea kuondoka askari wote wa kigeni katika ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Mustafa al-Kadhimi, waziri Mkuu wa Iraq Jumatatuu ijayo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Rais Joe Biden wa Marekani ambapo safari hiyo inalenga kufanyika mazungumzo baina ya pande mbili huku ajenda kuuu ikiwa ni uwepo wa wanajeshi wa Marekani huko Iraq.

Wabunge wa Iraq wanasisitiza kuwa, kuendelea kuwepo nchini hjumo mwanajeshi wa Marekani maana yake ni kukiukwa mamlaka ya kujitawala nchi hiyo.

Tags