Jul 27, 2021 15:10 UTC
  • Kwa msaada wa askari wa Israel, walowezi wa Kizayuni wauvamia tena msikiti wa Al Aqsa

Walowezi wa Kizayuni waliokuwa wakilindwa na kusindikizwa na askari wa utawala haramu wa Israel leo wameuvamia tena msikiti wa Al Aqsa katika mji mtukufu wa Baitul Muqaddas (Jerusalem).

Katika mwendelezo wa hatua zao za kiuadui na kishenzi dhidi ya matukufu ya Wapalestina, walowezi wa Kizayuni wameuvamia na kufanya vitendo vya kishenzi katika msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Ripoti kutoka Baitul Muqaddas zinaeleza kuwa, baada ya kuvamia uwanja wa msikiti huo, walowezi hao walianza kutoa nara na kaulimbiu dhidi ya Uislamu.

Mapigano na makabiliano makali yametokea baina ya walowezi hao wa Kizayuni na Wapalestina kufuatia uvamizi huo dhidi ya msikiti wa Al Aqsa.

Walowezi wa Kizayuni wakisindikizwa na askari wa utawala haramu wa Israel

Uvamizi huo wa leo umefanywa wakati makundi ya muqawama ya Palestina yalikwisha toa onyo hapo kabla kwa askari wa utawala pandikizi wa Israel na walowezi wa Kizayuni unaowaunga mkono, juu ya kurudia tena kufanya hujuma na uvamizi katika msikiti wa Al Aqsa na yakatangaza kwamba, kama yalivyofanya katika mapambano ya "Upanga wa Quds", kuanzia sasa yataitika na kutoa jibu la Labbayka kwa wito wa matukufu ya Palestina kwa kuzilenga na kuzishambulia ngome za Israel.

Kitambo si kirefu nyuma, walowezi wa Kizayuni walikivamia kitongoji cha Jabal Sabih kilichoko kwenye eneo la Beita katika Ufukwe wa Magharibi kwa lengo la kujenga kitongoji chao haramu, lakini maandamano ya Wapalestina na hatua waliyochukua ya kuanzisha mapambano iliwalazimisha wazayuni hao kuondoka katika eneo hilo.../

Tags