Jul 28, 2021 03:25 UTC
  • Wazayuni wakasirika kwa

Duru za habari za lugha ya Kiebrania zimetangaza kuwa kususiwa wanamichezo wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020 kumewakasirisha na kuwashtusha viongozi wa utawala huo haramu.

Gazeti la Kiebrania la Yediot Ahronot limeandika katika toleo lake la jana kuwa, viongozi wa utawala wa Kizayuni wameudhika mno kutokana na mtindo uliojitokeza wa kuwasusia wanamichezo wa utawala huo ulioanzishwa na wanamichezo wa nchi za Kiarabu katika mashindano ya Olimpiki.

Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti hilo, mwanamichezo Mualgeria Fat-hi Nurin alikataa kupambana na mwanamichezo Muisraeli katika mchezo wa judo; na kocha wake Ammar bin Khalif, alilielezea suala hilo: "katika upigwaji wa kura hatukuwa na bahati, kwa sababu mshindani wetu aliangukia kuwa Muisraeli, na kwa hivyo tukalazimika kujitoa." 

Gazeti la Yediot Ahronot limeashiria pia kujitoa katika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020  Muhammad Abdurasul, mwanajudo kutoka Sudan ambaye naye pia alikataa kupambana na mshindani wake Muisraeli na likaandika kuwa, kwa hakika hatua ya mwanajudo huyo Msudani imefelisha mchakato wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Sudan.

Wanamichezo wa nchi za Kiarabu wakitangaza mshikamano na Palestina kwa bango lililoandikwa "Palestina imo ndani ya nyoyo zetu"

Kwa mujibu wa gazeti hilo la Kiebrania, historia imethibitisha kuwa ukweli hauwezi kubadilishwa na kwamba mapatano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu yako makaratasini tu, lakini katika mazingira halisi ya mahusiano ya kiutu, wanamichezo wa nchi za Kiarabu wamethibitisha kuwa, kwa mtazamo wao, hakuna nchi inayoitwa Israel.

Wakati huohuo tovuti ya habari ya Araby21 imeripoti kuwa, wanamichezo wa nchi za Kiarabu wanaudhihaki utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwa kuendeleza mwenendo huo.../

 

Tags