Jul 31, 2021 02:40 UTC
  • Jenerali Joseph Aoun
    Jenerali Joseph Aoun

Kamanda wa jeshi la Lebanon amesisitiza kuwa vikosi vya jeshi hilo vipo tayari katika maeneo ya mipakani kwa ajili ya kukabiliana na hatari ya utawala wa Israel.

Jenerali Joseph Aoun amesisitiza kuwa, vikosi vya jeshi la Lebanon vitaendelea kuwa macho kwenye mipaka ya nchi ili kukabiliana na hatari yoyote ya adui huyo. Kamanda wa jeshi la Lebanon ameeleza hayo huko Beirut  akihutubia hafla ya maadhimisho ya mwaka wa 76 wa kuasisiwa jeshi la Lebanon. 

Jenerali Aoun ameashiria hali isiyoridhisha ya Lebanon iliyotokana na mgogoro wa kiuchumi na kifedha na janga la corona na kusema, macho na masikio yote yameelekezwa katika taasisi ya jeshi ambayo ni nukta ya matumaini kwa Walebanon licha ya migogoro yote mtawalia inayoikabili Lebanon na kushatadi kila uchao. 

Jenerali Aoun amevihutubu vikosi vya jeshi akisema kwamba: Msimruhusu yoyote atilie kutumia vibaya hali mbaya ya sasa ya kimaisha kwa ajili ya kuzusha shaka kuhusu imani na uzalendo wenu kwa sababu Lebanon ni amana iliyoko mikononi mwetu." 

Lebanon imetuma barua kadhaa kwa Umoja wa Mataifa ikilalamikia uvamizi na chokochoko mtawalia za wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel za kuingia kinyume cha sherfia katika anga ya nchi hiyo na kuutahadharisha utawala huo kwa kupuuza azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo lilitolewa na Baraza la Usalama mwaka 2006 kwa lengo la kuhitimisha vita vya siku 33 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon. Azimio hilo lilipelekea kutangazwa usitishaji vita baina ya Lebanon na utawala wa Kizayuni. 

Wanajeshi wa Israel katika vita vya siku 33 dhidi ya Lebanon mwaka 2006 

 

Tags