Aug 20, 2021 08:06 UTC
  • Wapalestina watakiwa wajitokeze kwa wingi katika kumbukumbu ya kuchomwa moto Msikiti wa Al Aqsa

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa mwito kwa Wapalestina kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya kukumbuka tukio la kuchomwa moto msikiti wa Al Aqsa.

Taarifa iliyotolewa na Hamas kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa 51 tangu msikiti wa Al Aqsa ulipochomwa moto imeeleza kwamba, msikiti huo ni mstari mwekundu kwa Wapalestina na ikawataka wananchi hao washiriki kwa wingi katika maandamano ya kukumbuka tukio la kuchomwa moto mahali hapo patakatifu.

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imesema: "Taifa letu litakata mikono ya watu wanaotaka kuuvunjia heshima msikiti wa Al Aqsa".

Harakati ya Hamas imeashiria pia kutiwa nguvuni na kuwekwa mbali na msikiti wa Al Aqsa Sheikh Raid Salah, kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Palestina katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel, na kueleza kwamba hatua hiyo ni njama iliyofanywa na adui Mzayuni ili kupadhibiti mahala hapo patakatifu.

Sheikh Raid Salah

Siku ya Jumanne wiki hii, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ulirefusha kwa muda wa miezi mingine sita kifungo cha fargha ilichomhukumu Sheikh Raid Salah, kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Palestina katika ardhi zilizoanza kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni mwaka 1948 na kupewa jina la Israel.

Tarehe 21 Agosti mwaka 1969, Msikiti mtukufu wa Al Aqsa, ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu na moja ya maeneo matakatifu yanayoheshimiwa na wafuasi wa kweli wa dini za mbinguni ulichomwa moto na kuharibiwa na Wazayuni.../

Tags