Aug 21, 2021 07:40 UTC
  • Syria: Mashambulizi ya Israel yana lengo la kuinua juu moyo wa magaidi

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Syria imelaani mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya ardhi ya nchi hiyo na kutangaza kuwa, lengo la hujuma hiyo ni kuinua juu moyo uliofifia na kukosa matumaini wa makundi ya kigaidi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imelaani mashambulizi hayo katika barua mbili tofauti zilizotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la umoja huo. Imesema kuwa, mashambulizi mapya ya Israel yanafanyika katika fremu ya siasa za utawala huo wa Kizayuni za kumwaga damu za watu wa Syria na kurefusha vita vya nchi hiyo dhidi ya makundi ya kigaidi. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema dunia inajua vyema kwamba, lengo la hujuma hiyo ni kuinua juu moyo uliopoteza matumaini wa makundi ya kigaidi na makundi ya waasi wanaoendelea kufanya uhalifu na jinai katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Syria yanayokaliwa kwa mabavu na Marekani na yale ya kaskazini magharibi yaliyovamiwa na majeshi ya Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan na vibaraka wao wa makundi ya kigaidi. 

Askari vamizi wa Marekani nchini Syria

Wizara ya Mambo ya Nchi za  Nje ya Syria imesema mashambulizi hayo yanakiuka sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa inayosisitiza kulindwa mamlaka ya kujitawala ya Syria. 

Vilevile imemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za umoja huo ili kuzuia hujuma na uhalifu wa Israel. 

Alkhamisi iliyopita Shirika la Habari la Syria (SANA) liliripoti kuwa kikosi cha anga cha nchi hiyo kimekabiliana na mashambulizi ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Tags