Sep 03, 2021 02:27 UTC
  • Mkuu mpya wa Shin Bet ya Israel aliongoza mauaji ya kamanda wa tawi la kijeshi la HAMAS

Kwa mara ya kwanza, gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot limetoa taarifa kuhusu mkuu mpya wa shirika la usalama wa ndani la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Shin Bet na kueleza kuwa, afisa huyo ndiye aliyeongoza mauaji ya kigaidi ya mwaka 2012 ya kamanda mwandamizi wa Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya HAMAS ya Palestina.

Wiki hii utawala wa Kizayuni wa Israel umeteua mkuu mpya wa Shin Bet atakayechukua nafasi ya Nadav Argaman anayestaafu.

Toleo la Alkhamisi la gazeti la Yediot Ahronot limemzungumzia mkuu huyo mpya wa shirika hilo la usalama wa ndani la Israel, ambaye kwa sasa anatambulishwa kwa herufi moja tu ya R.

Ripoti ya gazeti hilo la Kizayuni imeeleza kuwa, kipindi cha uongozi wa Argaman kinamalizika katika muda wa karibu mwezi mmoja na nusu ujao na mkuu mpya wa Shin Bet atashika wadhifa huo; na baada ya hapo utakapopita muda usiopungua wiki mbili itaruhusiwa kutangaza jina na kuonyesha picha ya mkuu huyo mpya wa Shin Bet.

Yediot Ahronot limeongeza kuwa, katika Intifadha ya Pili ya Wapalestina ya mwaka 2000, mkuu huyo mpya wa shirika la usalama wa ndani la utawala wa Kizayuni alihudumu katika vikosi muhimu vya utawala huo na mnamo mwaka 2012 aliongoza mauaji ya Ahmad al-Ja'bari, kamanda mashuhuri wa brigedi za Izzuddinu-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS.

Itakumbukwa kuwa, tarehe 14 Novemba 2012, Intifadha ya Pili ya Palestina au "Vita vya Siku Nane" ilianza, baada ya mauaji hayo ya kigaidi ya Ahmad al-Ja'bari, kamanda mwandamizi wa tawi la kijeshi la Hamas yaliyofanywa na utawala khabithi wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.../

Tags