Sep 03, 2021 11:45 UTC
  • Tathmini kuhusu hatua ya Marekani kuondoka katika vituo vyake vitatu vya kijeshi Syria

Marekani imeondoka katika vituo vyake vitatu vya kijeshi vilivyoko katika mikoa ya Deir ez-Zor na Al-Hasakah nchini Syria.

Baada ya hatua ya kijinai ya Marekani mnamo 3 Januari 2020 ambapo iliwaua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu  (IRGC) na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa Kikosi cha Hashd al Shaabi cha Iraq karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, maudhui ya kuondoka wanajeshi wa Marekani katika eneo iligeuka na kuwa takwa la wananchi katika aghalabu ya nchi za eneo. Nukta hii hasa imekuwa ikisisitizwa sana huko Iraq na Syria.

Pamoja na hayo, cheche ya kuondoka wanajeshi wa Marekani katika eneo imeanzia huko Afghanistan ambapo, hatimaye  tarehe 31 Agosti askari wa Marekani walimaliza rasmi oparesheni ya kuondoka nchini humo baada ya kuikalia kwa mabavu kwa muda wa miaka 20. Kwa kuzingatia kuwa Marekani haikufikia malengo iliyokuwa imeyataka nchini Afghanitan kama vile kukabiliana na ugaidi, kuinua kiwango cha haki za binadamu na kuanzisha katika nchi hiyo serikali thabiti, hatua yake ya kuondoka nchini humo bila kuwajibuka imepelekea Washington ipoteze itbari yake kimataifa. Nukta hii inapata nguvu hasa ikizingatiwa kuwa katika hujuma ya hivi karibuni dhidi ya uwanja wa ndege wa Kabul ambapo askari 13 wa Marekani waliuawa, ilibainika kuwa Washington haikuwa na uwezo wa hata kuwalinda askari wake yenyewe waliokuwa wakiondoka Afghanistan.

Aidha hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2021, Marekani inatazamia kuwa itakuwa imewaondoa askari wake nchini Iraq kwa mujibu wa mapatano baina ya Rais Biden wa Marekani na Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa Al Kadhimi. Kwa mujibu wa mapatano hayo, ni washauri wa kijeshi tu ndio watakabaki Iraq kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

Askari wa Marekani akiwa na wanagambao wa Kikurdi wa SDF nchini Syria

Kufungwa vituo vitatu vya kijeshi ambavyo vilikuwa Syria kinyume cha sheria ni ishara kuwa yamkini wakuu wa Washington wamekubali kuwa wameshindwa na kugonga mwamba katika malengo yao katika nchi hiyo ya Kiarabu na hivyo wameaumua kufunga vituo hivyo.

Kadhia ya Syria ni tofauti na Iraq na Afghanistan. Marekani imekuwepo Afghanistan katika kipindi cha miongo miwili iliyopita lakini uwepo wake Syria ni wa chini ya muongo moja. Kwa hivyo malalamiko dhidi ya Marekani na matakwa ya kuitaka iondoke Syria yana nguvu kuliko nchi hizo mbili tulizozitaja.  Marekani ilituma wanajeshi Syria kwa lengo la kubadilisha mfumo wa utawala nchini humo ili kuwaunga mkono wanamgambo wa Kikurdi kaskazini na kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya Kiarabu. Lengo la Marekani lilikuwa ni kuibua mfumo wa utawala wa majimbo wa kifederali na kuidhoofisha serikali kuu yenye makao yake Damascus. Mbali na hayo, Marekani pia iliwaunga mkono wanamgambo wa Kikurdi katika kupora mafuta ghafi ya petroli ya Syria na kuizuia serikali ya Damascus kunufaika na mali asili hiyo muhimu. Vitendo hivyo vya Marekani vimepelekea ichukiwe sana nchini Syria.

Nukta muhimu ni hii kuwa, Marekani ina vituo 13 vya kijeshi nchini Syria na kwa sasa imeondoka katika vituo vitatu tu. Hivyo hatuwezi kusema kuwa inalenga kuondoka kikamilifu nchini Syria.  Sababu ya kimsingi ya uwepo askari vamizi wa Marekani nchini Syria inaonekana kuwa ni kwa ajili ya usalama wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unapakana na Syria na Lebanon. 

Imearifiwa kuwa, Marekani imeondoka katika vituo vyake vitatu vya kijeshi katika maeneo ya Deir ez-Zor na Al-Hasakah nchini Syria baada ya kushindwa kuwasaidia Wakurdi kuunda mfumo wa kifiderali na hivyo imeamua kuwaacha wajishughulikie wenyewe.

Rais Biden wa Marekani

Katika upande mwingine, hatua hiyo ya Marekani nchini Syria imechukuliwa katika hali ambayo magaidi wa ISIS wameimarisha harakati zao tena katika eneo la kaskazini mwa Syria ambapo wametekeleza oparsheni karibu 18 za kigaidi Deir ez Zor hivi karibuni. Hivyo inaelekea kuwa Marekani imewapa uwanja magaidi hao waendeleze hujuma zao na nukta hii inaipa nguvu dhana kuwa Washington inawaunga mkono magaidi hao kinyume na madai yake kuwa inakabiliana nao.

Kwa vyovyote vile hata kama Marekani imeondoka Syria ili kupunguza gharama za kijeshi au kwa ajili ya sababu nyingine,  kilicho wazi ni kuwa itibari ya kijeshi ya Marekani imezidi kudhoofika na hii ni maudhui ambayo majenerali wastaafu Marekani wameikiri hivi karibuni.

Majenerali 90 wastaafu Marekani katika barua kwa rais wa nchi hiyo Joe Biden,  wamesema mbinu iliyotumika na nchi hiyo kuondoka Afghanistan imetoa pigo kubwa kwa itibari ya Marekani hasa machoni mwa waitifaki wake na hivyo wametaka Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Komandi ya Majeshi ya Marekani wajiuzulu.

Tags