Sep 05, 2021 02:40 UTC
  • Russia: Jeshi la Syria limetungua makombora 21 kati ya 24 ya Israeli

Jeshi la Russia linasema makombora ya ulinzi wa anga ya Jeshi la Syria yametungua aghalabu ya makombora ya Israeli yaliyokuwa yamevurumishwa kuelekea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus hivi karibuni.

Taarifa ya Jeshi la Russia imesema: "Takribani saa saba na nusu Septemba 3, ndege nne za kivita za Jeshi la Anga la Israeli aina ya F-15 zilivurumisha  makombora 24 yaliyolenga Jamhuri ya Kiarabu ya Siria kutoka anga ya Lebanon."

Admeri Vadim Kulit, naibu mkuu wa Kituo cha Maridhiano cha Russia kwa ajili ya  Syria, ametoa taarifa hiyo na kuongeza kuwa mifumo wa makombora ya angani ya anga-kwa-anga ya Buk-M2E na Pantsir-S1, ambayo imeundwa Russia, ilitumiwa na Jeshi la  Syria katika kutungua makombora hayo ya kisasa kabisa ya Israel.

Shirika rasmi la habari la Syria limenukuu duru za kijeshi nchini humo zikiripoti kuwa, ndege za kivita za Israel zilivurumisha makombora kadhaa kutoka upande wa Lebanon lakini aghalabu ya makombora hayo alitunuguliwa yakiwa angani na hivyo hayakuweza kulenga yalikokosudiwa.

Muda mfupi baada ya tukio hilo, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israeli viliripoti kuwa wakazi wa Tel Aviv, Ramat Gan na eneo jirani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) walisikia kwa uchache mlipuko mmoja.

Makombora ya Buk-M2E ya Jeshi la Syria ambayo yametumika kutungua makombora ya Israel

Jeshi la Israeli limesema linachunguza ikiwa milipuko hiyo ilisababishwa na kombora la Syria la ambalo huenda lilikuwa linalenga kombora la Israel.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imelaani shambulio la utawala wa Israeli katika ardhi ya Syria ikisema vitendo hivyo vya uchokozi vya utawala wa Tel Aviv havitaathiri azma ya nchi hiyo ya Kiarabu katika vita dhidi ya ugaidi.

Lebanon pia hivi karibuni iliwasilisha mashtaka Umoja wa Mataifa ikilalamikia hatua ya utawala haramu wa Israel kukiuka anga yake mara kwa mara wakati wa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Syria.

Utawala haramu wa Israel ni muungaji mkono mkubwa wa magaidi ambao wanataka kuiangusha serikali halali ya Rais Bashar al Assad nchini Syria.

Tags