Sep 07, 2021 11:12 UTC
  • Jibu kali la Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen kwa mawaziri wenzake wa Marekani na Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amezitaka Marekani na Uingereza kutoa mchango chanya na kutoegemea upande wowote katika juhud za kurejesha amani huko Yemen.

Akijibu matamshi ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Uingereza waliotaka Yemen itekeleza usitishaji vita haraka iwezekanavyo. Hesham Sharaf amesema kuwa matamshi hayo yanapasa kuelekezwa kwa nchi vamizi ambazo zinaendelea kuishambulia kwa mabomu, kuzizingira bandari na viwanja vya ndege vya Yemen na kuzuia kuingia nchini humo meli za mafuta na dawa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ameitaja misimamo ya Washington na London kuwa ni ya kisiasa na yenye lengo la kuuridhisha utawala wa Saudi Arabia ili uendelee kununua silaha za nchi hizo. 

Hesham Sharaf pia amesisitiza juu ya umuhimu wa kuchukuliwa hatua kama hizo za kibinadamu na za dharura ili kujenga hali ya kuaminiana na kurekebisha hali ya mambo. Amesema, kuna haja ya kuanza kuchukua hatua za lazima ili kufanikisha usitishaji vita wa pande zote na kufikia ufumbuzi wa kisiasa wa kiadlifu na kurejesha amani huko Yemen. 

Baada ya jeshi la Yemen hivi karibuni kutekeleza kwa mafanikio oparesheni katika ardhi ya Saudia kwa jina la "Seventh deterrent balance"; Washington na London zimelaani oparesheni hiyo na kuitaka Sana'a iafiki usitishaji vita kamili na wa haraka na ifanye juhudi za kuhitimisha mapigano huko Yemen kwa njia za kidiplomasia katika fremu ya  mazungumzo na Umoja wa Mataifa. Hii ni katika hali ambayo Saudi Arabia takriban kila siku inakiuka usitishaji vita kwa hatua yake ya kuyashambulia maeneo mbalimbali ya Yemen. 

Jeshi la Yemen 

 

Tags