Sep 09, 2021 07:32 UTC
  • Mateka wa Palestina wachoma moto jela nyingine ya Kizayuni

Duru za utawala wa Kizayuni zimetangaza kuwa, mateka wa Palestina wamechoma moto jela ya pili ya utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Shahab, duru hizo za Kizayuni zimethibitisha habari ya kuchomwa moto jela ya pili ya Kizayuni ya Ramon.

Shirika la Kijasusi na la Usalama wa Ndani la Israel limesema kuwa limejiandaa kwa ajili ya kukabiliana na uasi na vitendo kama hivyo katika jela za utawala wa Kizayuni hasa baada ya Wapalestina sita kutoroka jela hivi karibuni. 

Kabla ya kuchoma moto jela hiyo ya pili, mateka Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ya Ktzi'ot walikuwa pia wamechoma moto vyumba walimowekwa.

Jela ya Gilboa ya utawala wa Kizayuni yenye ulinzi mkali. Pamoja na hayo Wapalestina 6 wamefanikiwa kutoroka kishujaa

 

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Arab48, mateka waliowekwa kwenye kitengo cha sita cha gereza la Ktzi'ot lililoko katika eneo la jangwani la Negeb wamevichoma moto vyumba kadhaa vya gereza hilo kulalamikia ukatili na ukandamizaji wa kinyama wanaofanyiwa na utawala huo dhalimu.

Jumatatu wiki hii,  mateka sita Wapalestina walifanikiwa kutoroka kwenye jela yenye ulinzi wa hali ya juu kabisa ya Gilboa kaskazini ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopachikwa jina bandia la Israel.

Baada ya vyombo vya usalama vya utawala wa Kizayuni kujaribu bila mafanikio kuwakamata Wapalestina hao, askari wa utawala huo dhalimu wamewatia nguvuni na kuwaweka kizuizini jamaa kadhaa wa familia za mateka sita hao waliotoroka jela ya Gilboa.

Tags