Sep 11, 2021 11:21 UTC
  • HAMAS: Wazayuni hawana ubavu wa kuizuia Gaza isiendeleze mapambano ya silaha

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, hatua ya utawala haramu wa Israel ya kuishambulia kwa mabomu Gaza haiwezi kulizuia eneo hilo lisiendeleze mapambano yake ya silaha dhidi ya adui Mzayuni.

Hazim Qassim, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema hayo wakati alipokuwa akizungumzia uvamizi na hujuma za hivi karibuni za wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kueleza kwamba, hujuma dhidi ya Gaza ni mwendelezo wa uvamizi wa Wazayuni dhidi ya Quds inayokaliwa kwa mabavu na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.

Afisa huyo wa ngazi za juu wa chama cha Hamas amebainisha kuwa, mashambulio ya mabomu ya jeshi la utawala vamizi wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza lengo lake ni kuvunja umoja wa Wapalestina ambao umeundika katika pande tatu za Gaza, Quds na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Hazim Qassim, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

 

Amesisitiza kuwa, njama hizo za utawala vamizi wa Israel hazitafanikiwa kwani Wapalestina wako macho na wameazimia kuendeleza mapambano yao dhidi ya adui Mzayuni hadi pale watakapokomboa ardhi zao zilizoporwa na Wazayuni.

Hayo yanajirii katika hali ambayo, vyombo hivyo vya habari vya Kizayuni vimewahoji wataalamu wengi wa Israel na wamekiri kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni lilishindwa vibaya katika vita vya hivi karibuni vya Ukanda wa Gaza.

Utawala wa Kizayuni umeizingira Gaza tangu mwaka 2006 hadi hivi sasa kwa kuifungia njia zote za kuingia na kutoka kwenye eneo hilo, lakini Wapalestina wamezidi kuwa imara kiny7ume kabisa na ndoto za Wazayuni.

Tags