Sep 15, 2021 12:57 UTC
  • Hatibu wa al Aqsa: Mapambano ya taifa la Palestina yamezima njama za Israel dhidi ya Al Aqsa

Hatibu wa Msikiti wa al Aqsa amesema kuwa mapambano na kusimama kidete kwa taifa la Palestina vimezima na kukwamisha njama za utawala haramu wa Israel za kuudhibiti kikamilifu msikiti huo.

Sheikh Ekrima Sa'id Sabri amesema mataifa ya Kiarabu yanapinga mwenendo wa tawala za nchi zao wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala ghasibu wa Israel na kuongeza kuwa, tukio la kuchomwa moto Msikiiti wa al Aqsa hapo mwaka 1969 lilionesha njama zinazofanywa na Israel za kutaka kutimzia ndoto yake ya kuudhubiti msikiti huo.

Sheikh Ekrima Sabri ameongeza kuwa, Israel imetumia vibaya matukio mbalimbali kwa ajili ya kuudhibiti Msikiti wa al Aqsa lakini njama hizo zimefeli kutokana na kusimama kidete na mapambano ya taifa la Palestina linalosisitiza kuwa msikiti huo ni milki ya Waislamu.

Sheikh Ekrima Sa'id Sabri 

Sheikh Ekrima Sa'id Sabri amewataka Waislamu kufanya jitihada za kuutetea na kuustawisah Msikiti wa al Aqsa na kibla chao cha kwanza. 

Katika wiki za karibuni walowezi wa Kizayuni wakisaidiwa na askari wa utawala haramu wa Israel wamezidisha hujuma na mashambulizi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na maeneo ya kandokando yake wakiwa na lengo la kuwalazimisha Waislamu kuyahama maeneo hayo.   

Tags