Sep 21, 2021 02:42 UTC
  • Abdulmaliki al Houthi: Saudi Arabia na Imarati ni vibaraka wa Marekani

Katibu Mkuu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa Saudi Arabia na Imarati ni nyenzo zinazotumiwa na Marekani.

Abdulmalik al Houthi ambaye alikuwa akizungumza kwa mnasaba wa madhimisho ya mwaka wa saba wa mapinduzi ya wananchi wa Yemen amesema mafanikio makubwa zaidi ya mapinduzi ya Septemba 21 ni kuzuia kusambaratika nchi na kusitisha udhibiti wa nchi vamizi. 

Katibu Mkuu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen ameongeza kuwa, mapinduzi ya Septemba 21 yameirejeshea Yemen heshima na uhuru. Amesema, Marekani inachukua hatua kwa maslahi ya Israel; na Israel ni wakala wa maalumu wa Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia. Amesema wanafanya jitihada za kukomboa nchi nzima ya Yemen  hadi  kuundwa serikali yenye nguvu nchini humo. 

Katibu Mkuu wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amesisitiza kuwa, kabla ya mapinduzi ya Septemba 21 balozi wa Marekani alikuwa akiidhibiti nchi hiyo na ubalozi wa Washington ulichukua nafasi ya Rais wa Yemen. Amesema Yemen ingegawanyika na kusambaratika kikamilifu iwapo mapinduzi yasingetokea na kambi za Marekani zingeongezeka nchini humo kwa ksingizio cha kupambana na mtandao wa kigaidi wa al Qaida. Amesema kwa sasa Yemen inalengwa kwa maslahi ya Marekani, utawala wa Kizayuni na Uingereza.  

Magaidi wa mtandao wa al Qaida