Sep 22, 2021 07:32 UTC
  • Msafara mpya wa malori ya mafuta kutoka Iran yamewasili Lebanon

Televisheni ya al Mayadeen imetangaza kuwa msafara mwingine wa malori yenye shehena ya mafufa kutoka Iran umewasili Lebanon baada ya kuvuka mpaka wa Syria.

Kwa mujibu wa al Mayadeen, msafara huo wa malori yenye mafuta kutoka Iran ambayo yamedhaminiwa kupitia harakati ya Hizbullah kwa lengo la kusaidia kutatua uhaba wa mafuta huko Lebanon tayari umewasili nchini humo. Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon hivi karibuni alisema kuwa meli moja iliyosheheni mafuta kutoka Iran ilikuwa inaelekea Lebanon.

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon  

Kufuatia kauli hiyo, Lebanon Alhamisi iliyopita ilitangaza kuwa msafara wa kwanza wa malori yaliyobeba mafuta kutoka Iran yamewasili Lebaon kupitia Syria na katika mpaka wa nchi kavu katika eneo la mpakani la Hermil hadi al Qusair. 

Misafara mitatu mingine ya malori ya mafuta kutoka Iran imewasili katika ardhi ya Lebabon masaa machache baada ya kuwasili msafara huo wa kwanza. Lebanon ilitumbukia katika uhaba mkubwa wa mafuta ikiwa ni natija ya mashinikizo ya Marekani tangu mwaka mmoja na nusu uliopita; hatua iliyopelekea kuharibika uchumi wa nchi hiyo na kuipelekea Hizbullah kuomba msaada kutoka Iran ili kupunguza mgogoro wa mafuta huko Lebanon. 

Tags