Sep 23, 2021 08:08 UTC
  • Khatibu wa al-Aqswa: Wazayuni wanataka kutwisha uhakika mwingine kuhusu Msikiti wa al-Aqswa

Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa amesisitiza kuwa, hatua ya Wazayuni ya kung'ang'a kuingia kinyume cha sheria katika Msikiti wa al-Aqswa inaweka wazi njama zao za kutaka kutwisha uhakika mpya kuhusiana na kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

Sheikh Ekrima Sa'id Sabri amesema kuwa, bila ya himaya na uungaji mkono wa wanajeshi vamizi wa Israel, walowezi wa Kizayuni hawawezi kuthubutu kuingia katika Msikiti wa al-Aqswa, na hilo linaonyesha kuwa, wanaogopa hasira za wakazi wa Quds ambao ndio wamiliki asili wa maeneo matakatifu katika mji huo.

Khatibu wa Msikiti wa al Aqswa amesisitiza kuwa, viongozi wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakitoa himaya na uungaji mkono kamili kwa walowezi wa Kizayuni ambao wamekuwa wakifanya hujuma mara kkwa mara na kuingia  katika Msikiti wa al-Aqswa na kulivunjia heshima eneo hhilo takatifu.

Vitendo vya chuki na uadui vya walowezi wa Kizayuni vimeendelea baada ya jana mamia ya walowezi hao wenye chuki na Uislamu kuuvamia Msikiti wa al-Aqsa ambao ndicho Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Wanajeshi wa Israel wakivamia Msikiti wa al-Aqswa

 

Sheikh Ekrima Sabri alinukuliwa pia majuzi akisema kuwa, kuwa, Israel imetumia vibaya matukio mbalimbali kwa ajili ya kuudhibiti Msikiti wa al Aqswa lakini njama hizo zimefeli kutokana na kusimama kidete na mapambano ya taifa la Palestina linalosisitiza kuwa msikiti huo ni milki ya Waislamu.

Katika wiki za karibuni walowezi wa Kizayuni wakisaidiwa na askari wa utawala haramu wa Israel wamezidisha hujuma na mashambulizi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na maeneo ya kandokando yake wakiwa na lengo la kuwalazimisha Waislamu kuyahama maeneo hayo.   

Tags