Sep 23, 2021 11:00 UTC
  • Mamluki wote wa wavamizi wa Yemen wajisalimisha kwa Ansarullah huko Abadiya

Mamuliki wote wa wavamizi wa Yemen wanaoongozwa na Saudi Arabia katika wilaya ya al Abadiya mkoani Marib wamejisalimisha kwa jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen.

Tovuti ya habari la "al Khabar al Yamani" imetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, mamluki wote wa wavamizi wa Yemen wamejisalimisha kwa jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen bila ya kupigana hata kidogo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya jeshi la Yemen kukata njia zote za kufikishiwa misaada mamluki wa utawala wa kiimla wa Saudi Arabia wilayani al Abadiya, mamluki wa wavamizi hao wamejisalimisha, jeshi la Yemen na kamati za kujitolea za wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu wamefanikiwa kuikomboa wilaya hiyo bila ya upinzani wowote kutoka kwa wanamgambo wa Abdu Rabuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kukimbilia Saudia.

Ansarullah katika mapambano ya ukombozi wa Yemen

 

Al Abadiya ni wilaya ya pili kubwa ya mkoa wa Yemen kukombolewa na jeshi la nchi hiyo katika kipindi cha siku moja. Kabla ya hapo jeshi la Yemen na kamati za kutolea za wananchi wa nchi hiyo walikuwa wamekomboa wilaya nyingine muhimu ya Harib ya mkoa huo wa Marib.

Wakati tunaandika habari hii, jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen walikuwa wanazidi kusoma mbele pia katika ukombozi wa wilaya ya al Juba ya mkoa wa Shabwa wa katikati ya Yemen.