Sep 25, 2021 02:34 UTC
  • Mafuta ya Iran yafufua sekta ya kilimo nchini Lebanon

Mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanayoendelea kutumwa nchini Lebanon yamefanikiwa kufufua sekta ya kilimo katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo na shughuli za kilimo za wakazi wa maeneo hayo zimeanza kunawiri tena.

Televisheni ya al Alam imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, mafuta ya Iran yanayotumwa nchini Lebanon yameleta neema kwa wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu wakiwemo wakulima wa maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ambao walikuwa katika mgogoro wa kilimo kwa kukosa nishati hiyo muhimu.

Salim Murad, Mkurugenzi wa Taasisi ya Jihadi ya Ujenzi ya kusini mwa Lebanon amesema, mafuta yana mchango mkubwa katika uzalishaji wa mazao ya kilimo kwani maji ni kitu cha msingi katika kilimo na haiwezekani kupandisha juu maji na kuyasambaza mashambani bila ya kuwa na mafuta.

Msafara wa mafuta ya Iran kwa ajili ya wananchi wa Lebanon

 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kazi kubwa ya wananchi wa kusini mwa Lebanon ni kilimo kwa ajili ya kuendeshea maisha yao na walikumbwa na mgogoro mkubwa baada ya kukosekana bidhaa muhimu ya mafuta.

Vikwazo vya Marekani vimesababisha migogoro mingi ikiwemo ya kiuchumi nchini Lebanon. Upungufu mkubwa wa mafuta ni moja ya masuala ambayo yaliwaletea matatizo mengi wananchi wa nchi hiyo. Hata hivyo kwa ubunifu wa Hizbullah ya Lebanon wa kudhamini mafuta kutoka nchini Iran na kuhakikisha bidhaa hiyo inafika salama nchini humo, umekuwa ni mkombozi kwa wananchi wa Lebanon.

Wiki iliyopita na sambamba na kuingia shehena za kwanza za mafuta ya Iran katika ardhi ya Lebanon, Waziri wa Kazi wa serikali mpya ya Lebanon, Muṣṭafá Bayram alisema kwamba, shehena hizo za mafuta zimevunja mzingiro wa muda mrefu na wa kidhalimu ambao Marekani ilikuwa imeiwekea Lebanon.

Tags