Sep 25, 2021 02:35 UTC
  • Mwana wa muasisi wa Israel autabiria maangamizi utawala wa Kizayuni

Mwana wa mwasisi wa Israel ambaye baba yake ndiye aliyetia saini tangazo la kuanzishwa dola hilo pandikizi mwaka 1948 na ambaye hivi sasa ni mpinzani mkubwa wa utawala wa Kizayuni anayepitisha siku za mwisho za umri wake, ameutabiria maafa utawala huo dhalimu unaokikalia kwa mabavu Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Arab Post, Yaacov Sharett, mwana wa kiume wa Moshe Sharett, waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni na waziri mkuu wa pili wa Israel amesema kuwa, utawala wa Kizayuni umezaliwa kutoka tumbo la shari na maasi na huo ni uhakika usiopingika.

Yaacov Sharett ambaye hivi sasa amekaribia kuingia katika umri wa miaka 95 amesema hayo kwenye mahojiano na gazeti la Kizayuni la Haaretz na kuongeza kuwa, amefikia umri alio nao kwa utulivu, hali yake ya kimaisha ni nzuri lakini ana hofu kubwa na mustakbali wa wajukuu zake.

Yaacov Sharett

 

Amesema, mimi nipo hapa (katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel), sina pengine pa kwenda. Kutokana na umri wangu siwezi kuhamia sehemu nyingine. Lakini kila siku naungama na ninakiri kwamba Israel ni utawala vamizi ambao unavamia na kushambulia ardhi za watu wengine.

Utawala pandikizi wa Kizayuni ulianzishwa mwaka 1948 kwa msaada wa wakoloni wa Uingereza. Wapalestina waliporwa ardhi za mababu zao na sehemu yake kuanzishwa dola pandikizi la Israel ambalo mpaka hii leo linaendelea kufanya jinai zisizo na kifani dhidi ya Wapalestina.

Tags