Sep 25, 2021 03:42 UTC
  • HAMAS yalaani vikao vya viongozi wa Palestina na mawaziri, wabunge wa utawala wa Kizayuni

Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amelaani vikao vinavyofanywa baina ya maafisa wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Hazem Qassim amesema, hatua ya viongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kukutana na kufanya mazungumzo na mawaziri wa Israel na wabunge wa bunge la utawala huo wa Kizayuni la Knesset inalenga kuanzisha uhusiano wa kawaida, hivyo ni ya kulaaniwa na haikubaliki.

Qassim ameongeza kuwa, kuendelea kwa vikao hivyo ni ishara kwamba Mamlaka ya Ndani ya Palestina inakazania kufuata njia inayopingana na muelekeo wa kitaifa; na ni jinai ya kitaifa na kimaadili.

Hazem Qassim

Msemaji wa Hamas amebainisha kwamba, mwenendo huo wa Mamlaka ya Ndani unazihamasisha baadhi ya pande katika eneo kuendeleza usaliti wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel.

Katika wiki za karibuni na licha ya upinzani wa wananchi wa Palestina, baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani akiwemo rais wake Mahmoud Abbas wamekuwa wakikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel.

Mbali na kulaani hatua hiyo, wananchi wa Palestina wametaka Abbas ajiuzulu wadhifa wake wa urais wa Mamlaka ya Ndani.../

Tags