Sep 25, 2021 07:19 UTC
  • Al Miqdadi: Marekani ikomeshe kuwepo kwake haramu kijeshi katika ardhi ya Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesisitiza kuwa, kuwepo kijeshi Marekani nchini humo ni haramu na kinyume cha sheria na inapasa Washington iondoke katika ardhi ya nchi hiyo haraka iwezekanavyo.

Faisal al Miqdad amesema Marekani inapaswa iondoke katika ardhi ya Syria, la sivyo itafikwa na balaa sawa na mabalaa yaliyoikumba huko Afghanistan na katika ardhi za nchi zingine.

Al Miqdad ameongeza kuwa, vikwazo visivyohimilika vya Marekani vinawadhikisha mno wananchi wa Syria na akautaka Umoja wa Mataifa utekeleze jukumu lake kuhusiana na suala hilo kwa kulinda hati ya umoja huo na misingi yake mikuu.

Askari wa jeshi vamizi la Marekani nchini Syria

Katika miaka ya karibuni Marekani imekuwa ni balaa katika eneo la Asia Magharibi, hususan nchini Syria kwa wananchi wa nchi hiyo, mbali na wizi na uporaji wa mafuta, ambao kabla ya Washington ulikuwa ukifanywa na kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) katika maeneo mbalimbali ya ardhi ya Syria.

Serikali halali ya Syria imesisitiza mara kadhaa kwamba, Marekani na magenge yenye mfungamano nayo hawana lengo jengine lolote lile kwa kuwepo kwao katika maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki ya nchi hiyo isipokuwa kupora mafuta; na hivyo imewataka wakomeshe kuwepo kwao kinyume cha sheria nchini humo.../

Tags