Sep 26, 2021 04:35 UTC
  • Kuwait: Palestina ingali maudhui kuu na ya msingi katika ulimwengu wa Kiislamu

Waziri Mkuu wa Kuwait amesema kuwa, Palestina ingali maudhui kuu na ya asili katika ulimwengu wa Kiislamu.

Sabah al-Khalid al-Sabah Waziri Mkuu wa Kuwait amesema hayo mjini New York Marekani katika hotuba yake kwenye mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa, madhali taifa la Palestina halijapata haki zake zote za kisheria na utawala haramu wa Israel unaendelea na hatua zake za kukiuka sheria za kimataifa na utu kama ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina, kupora ardhi, kubomoa nyumba zao na kuyavunjia heshima maeneo matakatifu, mizozo na mivutano itaendelea kushuhudiwa katika eneo la Asia Magharibi.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Kuwait ametoa wito wa kupatiwa ufumbuzi kadhia ya Palestina ili wananchi hao waweze kuishi kwa usalama na amani katika ardhi zao.

 

Waziri Mkuu wa Kuwait amesisitiza udharura wa kuundwa nchi huru ya Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas sambamba na kurejea wakimbizi wa Kipalestina katika ardhi zao za asili.

Sabah al-Khalid al-Sabah amesema katika hotuba yake hiyo kwamba, mgogoro wa Yemen ni tishio kwa amani na usalama wa eneo la Asia Magharibi na kusisitiza kwamba, msimamo wa Kuwait ambao ni thabiti na usiotetereka ni kuwa, ufumbuzi pekee wa mgogoro wa Yemen ni njia za kisiasa.

Tags