Sep 26, 2021 08:02 UTC
  • Serikali ya Kurdistan yalaani mkutano wa Erbil wa kuanzisha uhusiano na Israel

Wizara ya Mambo ya Ndani ya eneo la Kurdistan la Iraq lenye utawala wa ndani sambamba na kusisitiza kuwa, itawachukulia hatua watu walioitisha na kuandaa mkutano wa jana wa Erbil kwa kupotosha malengo ya mkutano huo na badala yake kuwa ni kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel imetangaza kuwa, eneo hilo linafungamana na sera rasmi za Wizara ya Mashauuri ya Kigeni ya Iraq kuhusiana na Palestina.

Taarifa ya serikali ya Kurdistan imebainisha kwamba, tunajitenga mbali kabisa na mkutano huo, hatukuwa na taarifa za malengo pamoja na maudhui ya mkutano huo na kilichojadiliwa katika mkutano huo, hakiakisi msimamo wa kisiasa wa eneo hilo.

Taarifa hiyo ya eneo la Kurdistan la Iraq lenye utawala wa ndani imekuuja baada ya kutolewa taarifa, radiamali na kuripotiwa upinzani wa kila upande nchini Iraq kufuatia mkutano huo wa amani wa Erbil ambao ulilebeba anuani ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimi nayo imetoa taarifa rasmi  na kulaani vikali mkutano huo wa Erbil.

Maandamano ya kupinga kuanzisha uhusiano wa kawaida na uutawala haramu wa Israel

 

Sayyid Ammar Hakim, Kiongozi wa Mrengo wa Kitaifa wa al-Hikma wa Iraq  ametoa taarifa katika radiamali yakke kuhusiana na mkutano huo akisema: Tunalaani mikutano na makongamano yanayofanyika nchini Iraqw na kutoa wito wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.

Kwa upande wake Sayyid Muqtada Sadr Kiongozi wa Harakati ya Al-Sadr ya nchini Iraq ameitaka serikali ya Baghdad kuwatia mbaroni washiriki wa mkutano huo.

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeripoti kuwa, takribani viongozi wa kikabila 300 huko Iraq wameshiriki katika mkutano wa Erbil wakitaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel.