Sep 27, 2021 04:33 UTC
  • Jeshi la Israel lapatwa kiwewe likihofia kisasi cha wanamapambano wa Palestina

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limejiweka katika hali ya tahadhari likihofiia kisasi kutoka kwa wanamuqawama wa Palestina na kuvurumishwa makombora kuelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Duru za habari za Kizayuni zimeripoti kuwa, Israel imejiweka katika hali ya tahadhari katika mipaka ya Ukanda wa Ghaza sambamba na kuiweka tayari ngao yake ya kujilinda na makombora ikihofia kuvurumishwa makombora kutoka Ukanda wa Ghaza kama jibu la oparesheni iliyofanywa na jeshi la utawala huo katika Ukingo wa Magharibi mwa Jordan.  

Wanajeshi wa Israel katika hali ya tahadhari 

Wanajeshi wa jeshi la utawala wa Kizayuni wakisaidiwa na askari kanzu, walivamia maeneo kadhaa katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan ikiwemo miji ya Jenin na Burqin na kukabiliana na wanamapambano wa Palestina. Katika mapigano hayo, askari kanzu hao wamewauwa shahidi Wapalestina watano na wanajeshi wawili wa Israel wamejeruhiwa. Hali ya wanajeshi hao imeripotiwa kuwa mbaya. 

Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa, upo uwezekano wa kuvurumishwa roketi kutoka Ukanda wa Ghaza. Wazayuni wamekumbwa na kiwewe na kujiweka katika hali ya tahadhari katika hali ambayo mfumo wa kujilinda na makombora wa Iron Dome umefeli katika vita vya Saifl Quds (Panga la Quds). 

Tags