Oct 05, 2021 02:22 UTC
  • Hizbullah: Mafuta ya Iran yamevunja mzingiro wa kiuchumi dhidi ya Lebanon

Mkuu wa Baraza la Utendaji la harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, kuingizwa Lebanon shehena ya mafuta kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kumevunja mzingiro wa kiuchumi dhidi ya Lebanon.

Sayyid Hashim Safiyuddin jana alieleza kuwa, Lebanon hii leo inakabiliwa na njama za Marekani, Magharibi na utawala wa Kizayuni na kwamba baadhi ya nchi za pambizoni mwa Ghuba ya Uajemi pia zinaisaidia Marekani katika kutekeleza njama hizo dhidi ya Lebanon. 

Safiyuddin ameongeza kuwa, Wazayuni wenyewe wamekiri kwamba hawawezi kuchukua hatua yoyote dhidi ya meli za mafuta za Iran zinazoelekea Lebanon na sababu yake ni kuwa Wazayuni hawakutaka kuingia katika vita vya baharibi na Hizbullah na hiyo ni nukta ya udhaifu ya utawala wa kizayuni na nukta nguvu kwa Hizbullah. 

Shehena za mafuta kutoka Iran kuelekea Lebanon 

Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, Wazayuni wanaelewa vyma kuwa makombora ya Hizbullah yana uwezo wa kufika mbali zaidi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel); kwa msingi huo ilikuwa wazi kuwa Wazayuni wasingeweza kushambulia shehena ya mafuta ya Iran iliyotumwa kwa watu wa Lebanon.

Tags