Oct 11, 2021 07:41 UTC
  • Nabil Abu Rudeineh: Utawala ghasibu wa Israel ni msingi wa ugaidi

Msemaji wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa utawala ghasibu wa Israel ni msingi wa ugaidi.

Akijibu leo matamshi ya karibuni ya Naftali Bennett Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Nabil Abu Rudeineh amesema: Nchi mbalimbali duniani zimeitambua nchi ya Palestina yenye mji mkuu wake Quds Mashariki; na kwamba tangu mwaka 2012 Palestina ni mwanachama mtazamaji wa Umoja wa Mataifa. Amesema Naftali Bennett hapaswi kupinga au kuafiki suala hilo kwa sababu wananchi wa Palestina kamwe hawatafumbia macho haki yao hiyo. 

Naftali Bennett Waziri Mkuu wa Israel 

Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni hivi karibuni alidai kuwa nchi ya Palestina haiwezi kuundwa kwa sababu itakuwa ya kigaidi. Abu Rudeineh ameongeza kuwa amani ya kweli itapatikana pale kutakapokomeshwa ukaliaji mabavu wa Israel katika ardhi na matukufu ya Palestina; na wananchi wa nchi hiyo watakapolinda na kutetea haki na matukufu yao. 

Msemaji wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza ulazima wa kufikiwa amani ya pamoja na ya kiadilifu ili kuhitimisha ukaliaji mabavu wa Maghasibu Wazayuni na kuasisi nchi huru ya Palestina na kubainisha kuwa: Palestina haitasalimu amri mbele ya haki zake.  

Tags