Oct 14, 2021 07:04 UTC
  • Jihad Islami: Mateka 150 wa Kipalestina wanafanya mgomo wa kula katika jela za Israel

Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa, mateka 150 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza za Israel walianza mgomo wa kula tangu jana Jumatano.

Msemaji wa Jihad Islami, Tariq Izzuddin amesema kuwa, kuanza mgomo huo wa matekani wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza na jela za Israel ni hatua muhimu katika vita vya Wapalestina hao dhidi ya mamlaka za magereza za Israel na taasisi za ujasusi za utawala huo.

Izzuddin ameongeza kuwa kuwatetea matekani ni wadhifa mtakatifu wa kitaifa na kusema kuwa, hatua zote za maandamano, mihadhara na harakati za aina tofauti ni huduma muhimu katika kupaza sauti ya kuwatetea mateka hao wanaokumbana na mashaka na manyanyaso makubwa. 

Zaidi ya watoto 170 wa Kipalestina wanashikiliwa katika korokoro za Israel

Amewataka wapenda haki wote kupaza sauti ya kuwatetea maelfu ya mateka wa Kipalestina wanaoishi katika mazingira mabaya kwenye jela na magereza za Israel.

Wapalestina karibu elfu 4 na 800 wanashikiliwa katika mahabusu za kutisha za utawala haramu wa Israel wakiwemo watoto 170.   

Tags