Oct 14, 2021 13:02 UTC
  • UNESCO: Hujuma na jinai za utawala wa Kizayuni Baitul Muqaddas ni batili

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema, Baitul Muqaddas (Jerusalem) ni mji unaokaliwa kwa mabavu; na hujuma na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya mji huo ni batili.

UNESCO imetoa sisitizo hilo katika kikao cha 212 cha baraza lake la utendaji kilichofanyika mjini Paris, Ufaransa na kuongeza kwamba, hujuma, mashambulio na jinai unazotenda Israel ndani ya mji huo ni batili.

Halikadhalika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni limetilia mkazo kusimamishwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, ikiwemo kuvamia na kukalia kwa mabavau ardhi zao, kujenga vitongoji vya walowezi katika ardhi hizo na kubomoa turathi za kale na za kihistoria za maeneo yote ya Palestina hususan katika mji wa Quds.

Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unaendeleza ujenzi haramu wa vitongoji kwa madhumuni ya kutaka kubadilisha muundo wa kijiografia wa maeneo ya Palestina kwa kuzayunisha na kuimarisha ubeberu na udhibiti wake katika maeneo hayo.

Ili kufanikisha malengo ya kujipanua ya utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel, askari wa utawala huo haramu kila siku wanashambulia na kuvamia maeneo mbalimbali ya Wapalestina na kuwatia nguvuni wananchi hao kwa kutumia visingizio bandia na madai hewa.../

Tags