Oct 15, 2021 14:00 UTC
  • Rais wa Lebanon amuonya kinara wa wanamgambo walilotekeleza mauaji Beirut

Rais wa Lebanon amebainisha masikitiko yake kutokana na mapigano na ufyatulianaji risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut jana huku akimuonya kiongozi wa kundi la wanagambo wa chama cha 'Vikosi vya Lebanon'.

Gazeti la Al Akhbar limeandika kuwa, punde baada ya ufyatulianaji risasi jana, Rais Michel Aoun wa Lebanon alimpigia simu Samir Geagea, kiongozi wa chama cha 'Vikosi vya Lebanon' na kumtahadharisha kushusu matukio hayo ya ufatulianaji risasi na kisha akamfahamisha bayana kuwa: 'Sitisha mchezo wako."

Gazeti hilo limeandika kuwa katika mazungumzo hayo, Geagea amedai kuwa wanamgambo wake hawakuhusika katika mauaji ya jana  mjini Beirut.

Katika hotuba baada ya tukio hilo, Rais Aoun alilaani vikali ufyatulianaji risasi katika eneo la At-T'ayyunah.

Samir Geagea

Jana asubuhi makundi ya watu wa Lebanon wanaopinga utendaji kazi wa Tariq Bitar mkuu wa uchunguzi wa mlipuko wa Beirut waliandamana  mbele ya jengo la Idara ya Mahakama ambapo ghafla walifyatuliwa risasi na watu wenye silaha. Katika tukio hilo watu saba waliuawa shahidi na wengine zaidi ya sitini kujeruhiwa.

Kufuatia tukio hilo, Harakati za Hizbullah na Amal zimetoa taarifa na kuwataka wananchi wa Lebanon wawe watulivu na wasikubali kutumbukizwa katika 'fitina khabithi' na kutangaza kuwa, walishiriki katika kuwashambulia waandamanaji wanafungamana na chama cha 'Vikosi vya Lebanon."

Tags