Oct 17, 2021 07:58 UTC
  • Abdulsalam: Marekani inashirikiana na al Qaida huko Ma'rib

Msemaji wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amesisitiza kuwa Marekani imedhihirisha kuwa ina mahusiano na kushirikiana na magaidi baada ya kutaka kufunguliwa vivuko eti vya amani huko Ma'rib.

Muhammada Abdulsalam amejibu taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuhusu hali ya mambo katika mkoa wa Ma'rib kwa kusema: Ombi la Marekani la kutaka kufunguliwa vivuko vya amani huko Ma'rib kwa kisingizio cha kutaka kuwapitisha majeruhi wa vita ni uthibitisho tosha kwamba Washington inashirikiana na magaidi katika eneo la al Abdiya mkoani Ma'arib.  

Kutekwa kambi ya kijeshi ya Saudia, moja ya mafanikio ya jeshi la Yemen dhidi ya Saudia mkoani Ma'rib

Abdulsalam ameeleza kuwa, Marekani inapiga nara za  uwongo kuhusu amani na kutaka kufunguliwa vivuko hivyo tajwa kufuatia kukaribia vikosi vya wanamuqawama katika vituo vya mwisho vya Saudia na mamluki wa kitakfiri huko Ma'rib. 

Hii ni katika hali ambayo Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani huko nyuma ilitoa taarifa ikitaka kufunguliwa vivuko eti vya amani huko Ma'rib. Wizara hiyo ilidai kuwa inafanya hivyo ili kuandaa uwanja kwa wanajeshi na majeruhi wote kuvuka kupitia vivuko hivyo vya amani.  

Wanamuqawama wa Yemen hivi karibuni walipata mafanikio mapya katika mapigano baina yao na mamluki wa Saudia mkoani Ma'rib. 

 

Tags