Oct 17, 2021 12:21 UTC
  • Baada ya mauaji kuongezeka, kundi la Taliban laahidi kulinda misikiti ya Mashia

Baada ya mashambulio ya kigaidi dhidi ya misikiti ya Mashia nchini Afghanistan kuongezeka, viongozi wa kundi la Taliban linalotawala nchini humo wametangaza kuwa, wataweza usalama na ulinzi katika misikiti ya Waislamu hao.

Abdul-Ghafar Muhammadi, Kamanda wa Polisi ya Taliban katika mji wa Qandar amesema kuwa, wamechukua hatua zaidi za kuimarisha amani na usalama katika misikiti ya Waislamu wa Mashia.

Uamuzi huo wa kundi la Taliban unachukuliwa baada ya kushuhudiaw kukithiri mashambulio ya kigaidi na milipuko katika misikiti ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan katika siku za hivi karibuni.

Makumi ya watu waliokuwa katika Swala ya Ijumaa waliuawa shahidi na wengine karibu ya mia moja walijeruhiwa katika milipuko miwili iliyotokea Ijumaa iliyopita katika Msikiti wa Bibi Fatima katika mji wa Qandahar Afghanistan. 

Jinai ya magaidi katika Msikiti wa Washia huko Qandahar, Afghanistan 

 

Ijumaa ya kabla ya hapo pia, Wiki iliyopita pia Waislamu wasiopungua mia moja waliuawa katika shambulizi la kigaidi lililolenga waumini waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala ya Ijumaa katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan na wengine karibu mia mbili walijeruhiwa. 

Kundi la kigaidi la daesh limetangaza kuhusika na mauaji na jinai hizo dhidi ya Waislamu wa Kishia.

Jumuiya ya Kutetea Wahanga wa Ugaidi yenye makao yake nchini Iran imetangaza kuwa, ugaidi umekuwa ukitumiwa kama fimbo na wenzo wa kulinda na kupanua maslahi ya madola ya kibeberu na wala hauna mfungamano na dini wala madhehebu yoyote ya dini.