Oct 18, 2021 12:21 UTC
  • Ongezeko la idadi ya wanajeshi watoro katika jeshi la Israeli

Duru za habari za Israel zimeripoti kuwa idadi ya askari wanaotoroka jeshi la utawala huo inaongezeka siku baada ya siku.

Tovuti ya lugha ya Kiebrania ya "Walla" imeripoti kuwa, mwaka huu wa 2021 pekee idadi ya askari wa Isael wanaozungumza lugha y Kiarabu waliotoroka kutokana na kubaguliwa na vilevile wanajeshi wa kawaida wanaotoroka huduma za jeshi, imeongezeka. 

Tovuti hiyo imewanukuu maafisa wa jeshi la Israel kwamba, miongoni mwa sababu za ongeeko la kutoroka wanajeshi hao ni ubaguzi unaoshuhudiwa ndani ya jeshi al Israel. 

Tovut ya Walla imeripoti pia kwamba sambamba na ongezeko hilo la kukimbia wanajeshi wa Israel, idadi ya askari wanaojiua katika jeshi hilo pia inatia wasiwasi. 

Visa vya kujitoa roho wanajeshi wa Israel vimeongezeka sana katika miaka ya karibuni na mwaka jana pekee kuliripotiwa makumi ya wanajeshi wa utawala huo haramu walioamua kujitoa uhai. 

Kumekuwepo malalamiko makubwa ndani ya jeshi la Israel dhidi ya ubaguzi unaofanywa dhidi ya baadhi ya makundi ya jeshi hilo.

Televisheni ya Israel imetangaza kuwa, makumi ya maafisa weusi wa jeshi la utawala huo wamemwandikia barua mkuu wa vikosi vya jeshi la Israel, wakimtaka achukue hatua za kukomesha ubaguzi na ubaguzi wa rangi unaoendelea kushika kasi zaidi katika muundo wa jeshi la utawala huo.

Mayahudi wa Ethiopia maarufu kwa jina la Mafalasha, waliorubiniwa kwenda katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, wamekuwa wakifanya maandamano ya kalalamikia unyanyasaji na ubaguzi wanaofanyiwa na Wazayuni. 

Tags