Oct 21, 2021 02:53 UTC
  • Baraza la Usalama lataka kusitishwa vita Yemen haraka iwezekanavyo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kusitishwa vita haraka iwezekanavyo huko Yemen katika kuunga mkono muungano vamizi na katili wa Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo.

Nchi wanachama  wa Baraza la Usalama jana usiku zilitoa taarifa zikitaka kusitishwa vira mara moja katika nchi nzima ya Yemen kwa mujibu wa azimio la baraza hilo nambari 2565 ili kulizuia jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen kuudhibiti mkoa wa Ma'rib.  

Taarifa hiyo ya nchi wanachama wa Baraza la usalama  imesisitiza juu ya ulazima wa kusitishwa mapigano ikiwemo kusitishwa mara moja kusonga mbele vikosi vya Yemen huko Ma'rib katikati mwa nchi hiyo. Nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa aidha zimedai katika taarifa hiyo kuwa,kutopiga hatua mchakato wa kusaka amani huko Yemen kunaweza kutumiwa vibaya na magaidi na kueleza wasiwasi wao kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili Yemen. 

Nchi wanachama wa Baraza la Usalama pia zimetangaza kumuunga mkono Hans Grundberg Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Yemen na kuzitolea mwito pande zinazozozana nchini humo kukukutana  na Grundberg chini ya usimamizi wa umoja huo. Itakumbukwa kuwa vikosi vya jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi katika wiki za hivi karibuni wamepata mafanikio makubwa ya kimaidani dhidi ya vikosi vamizi na mamluki wao katika mapigano huko Ma'rib. 

Vikosi vya Yemen katika mapigano mkoani Ma'rib