Oct 21, 2021 07:19 UTC
  • Wanajeshi karibu 20 wa Saudi Arabia waangamizwa nchini Yemen

Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimetangaza kuwa wanajeshi karibu 20 wa nchi hiyo wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika shambulizi la makombora lililofanywa na jeshi la Yemen.

Ripoti za vyombo vya habari vya Saudi Arabia zinasema kuwa, wanajeshi hao wameangamizwa katika shambulizi lililofanyika mapema leo Alkhamisi dhidi ya ngome za askari vamizi katika eneo la Abu Arish katika mkoa wa Jizan nchini Saudi Arabia. Maaafisa 6 na wanajeshi wasiopungua 12 wa Saudia wameangamizwa katika hujuma hiyo na makumi ya wengine wamejeruhiwa. 

Wanaharakani wa Saudi Arabia wamefichua kwamba, ndugu zao ambao ni maafisa na wanajeshi katika jeshi la nchi hiyo pia wamengamizwa katika hujuma hiyo ya makombora ya wapiganaji wa Yemen. 

Mapema jana pia makamanda wanne wa ngazi za juu wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia huko Yemen waliangamizwa katika katika mapigano wapiganaji wa Yemen.

Shirika la habari la IRNA limevinukuu vyombo vya habari vya muungano vamizi wa Yemen vikitangaza kuwa, Masoud al Sayyad, mkuu wa operesheni wa brigedi ya 143 ya wapiganaji wa nchi kavu wa muungano huo pamoja na Abdul Raqim al Naqash, Ibrahim Ali Naji al Hijri na Wasim Taufiq Ali wameuawa katika vita vinavyoendelea kwenye mkoa wa Ma'rib baina ya muungano huo vamizi na jeshi la Yemen linaloshirikiana na kamati za ukombozi za kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo.