Oct 25, 2021 02:31 UTC
  • Sisitizo la Pakistan la kutokuweko makubaliano baina yake na Marekani ya operesheni za kijeshi nchini Afghanistan

Serikali ya Pakistan imekanusha ripoti za vyombo vya habari zinazoeleza kufikiwa makubaliano kati yake na Marekani kwa ajili ya kufanya operesheni za kijeshi na kijasusi nchini Afghanistan.

Asim Iftikhar, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Pakistan ametangaza kuwa, hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kati ya Islamabad na Washington ya kutumia anga ya Pakistan kwa ajili ya kutekeleza operesheni ya kijeshi nchini Afghanistan. Hii ni katika hali ambayo, kabla ya hapo, Kanali ya Televissheni ya CNN ilikuwa imeripoti kuwa, serikal;i ya Marekani imo katika mazungumzo na viongozi wa Pakistan kwa ajili ya kupatiwa kituo cha anga cha nchi hiyo ili ikitumie kwa ajili ya kufanya doria na kukusanya taarifa za kijeshi nchini Afghanistan.

Kabla ya hapo, Imran Khan Waziri Mkuu wa Pakistan na nyota wa zamani wa mchezo wa kriketi alisema kuwa, historia ya uhusiano wa Pakistan na Marekani katika kipindi cha miongo miwili iliyopita ni  ya kutisha na ni ya maafana akaeleza bayana kwamba, Pakistan ikiwa muitifaki wa Marekani imeshambuliwa mara chungu nzima na ndege zisizo na rubani za Washington. 

Suala la jeshi la Marekani kupatiwa kituo cha anga nchini Pakistan ni miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakijadiliwa na duru za kisiasa na habari kkatika eneo baada ya Marekani kuondoa majeshi yake huko nchini Afghanistan; hata hivyo maafisa wa kijeshi na kisiasa wa Islamabad wanakusha kabisa kuhusu kuweko mpango kama huo.

Asim Iftikhar, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Pakistan

 

Baada ya Rais Joe Biden wa Marekani kuchukua uamuzi wa kuondoa majeshi ya nchi yake nchini Afghanistan kufikia Septemba 2021, kuliibuka tetesi mbalimbali kuhusiana na mpango wa Whitye House wa kujenga au kupatiwa kituo cha kijeshi nchini Pakistan.  Maafisa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na kijeshi wa Marekani pasi na kuashiria jina la Pakistan walisisitiza kwamba, ili kuweko na usimamizi na uangalizi kwa Afghanistan, kuna haja ya sehemu ya wanajeshi wa nchi yake kubakia katika vituo vya kijeshi vilivyoko jirani na Afghanistan. Kutokana na sababu mbalimbali, wengi waliamini kwamba, jirani aliyekusudiwa ni Pakistan. Hasa kwa kutilia maanani kwamba, kabla ya wanajeshi wa Marekani kuanza kuondoka nchini Afghanistan, kulienea taarifa za kuhamishiwa nchini Pakistan baadhi ya zana za kijeshi na suhula za vita za jeshi la Marekani.

Suala la kurejea tena Marekani nchini Pakistan kwa malengo yya kijeshi na kiintelijensia kutokana na kuwa na faili chafu na haribifu baina ya wananchi wa nchi hiyo lina unyeti mkubwa kiasi kwamba, baada tu ya kuenea habari ya kutaka kuweko tena jeshi la Marekani huko nchini Pakistan, viongozi wa Islamabad walijitokeza haraka na kukanusha hilo ili kuepusha aina yoyote ile ya malalamiko au mzozo wa kijamii kuhusiana na kadhia hiyo.

Rais Joe Biden wa Marekani

 

Miaka 9 iliyopita, Marekani ililazimika kukabidhi kituo chake cha mwisho cha kijeshi nchini Pakistan kwa serikali ya nchi hiyyo, ambapo hilo lilikuwa moja ya matakwa makuu ya wananchi wa nchi hiyo kwa viongozi na watawala wa nchi kwa minajili ya kuratibu uhusiano na Washington.

Katika hali ambayo, katika kipindi cha takribani miezi mitatu iliyopita hadi sasa kumefanyika mazungumzo baina ya viongozi waandamizi wa kisiasa na kijeshi wa Islamabad na Washington kuhusiana na matukio ya Afghanistan, kwa mara nyingine tena kumeibuka tetesi kuhusiana na kutumia Marekani ardhi  ya Pakistan kwa ajili ya kutekeleza operesheni za kijeshi na kiintelijensia nchini Afghanistan, suala ambalo limegonga vichwa vya habari za duru mbalimbali.

Kuna uwezekano kwamba, Pakistan ikiwa na nia ya kupata himaya ya kisiasa ya ikulu ya Marekani White House katika uga wea ushindani wa kieneo na India, na vilevile kupata misaada ya kifedha na kijeshi kutoka kwa Marekani imefikia makubaliano ya siri na nchi hiyo na hivyo kuandaa uuwanja na mazingira ya kutumiwa ardhi yake na asasi za kiintelijensia za Marekani kwa ajili ya kufanya ujasusi nchini Afghanistan, ambapo kama hilo litakuwa na ukweli, basi linaweza kuwa changamoto kubwa mno kwa serikali ya Waziri Mkuu, Imran Khan.

Tags