Oct 26, 2021 08:03 UTC
  • Wasyria waandamana kushinikizi kuondoka vikosi vamizi vya Uturuki

Mamia ya wananchi wa Syria wamefanya maandamano katika mkoa wa Aleppo (Halab), kaskazini magharibi mwa nchi kulaani uwepo wa wanajeshi vamizi wa Uturuki katika ardhi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la SANA, wakazi wa mji wa Kafr Naya katika mkoa wa Aleppo jana alasiri walimiminika katika barabara na mitaa ya mji huo wakitaka kuondoka nchini humo jeshi vamizi la Uturuki linaloshirikiana na magenge watifaki ya kitakfiri.

Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba bendera za Syria wamesema wanajeshi wa Uturuki wakishirikiana na mamluki wao wanashambulia makazi ya raia na miundombinu katika mji wao, hivyo wanapaswa kuondoka nchini humo mara moja.

Mapema mwezi huu, Ibrahim Kalin, msemaji wa rais wa Uturuki alidai kuwa, nchi hiyo, kama zilivyo Russia na Marekani, ina haki ya kuwepo kijeshi katika ardhi ya Syria. Alidai kuwa nchi yake haina tamaa ya kitu chochote katika ardhi ya Syria, lakini imelazimika kuchukua hatua kama hiyo kwa ajili ya usalama wake.

Uwepo wa kijeshi wa Uturuki nchini Syria

Hayo yanajiri wakati serikali ya Syria imeshatangaza mara kadhaa kuwa, uwepo kijeshi wa Marekani na Uturuki katika ardhi ya nchi hiyo ni wa kivamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu na kusisitiza kwamba, nchi hizo mbili zinapaswa kuondoka katika ardhi ya Syria. 

Lakini kinyume na Marekani na Uturuki, Russia iko kijeshi nchini Syria kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kupambana na ugaidi na makundi yanayobeba silaha.

Tags